Friday, March 12, 2010

Naanza na mchongoma


katuni hii inapatikana katika gazeti la Semausikike

Monday, March 8, 2010

Sunday, March 7, 2010


Umeliona pozi langu,nilikuwa kwetu nilikozaliwa katika mkoa wa Iringa

Saturday, March 6, 2010

Kumekuchwa,(Machweo)

Jua ndio linazama hivyo. Biashara asubuhi jioni mahesabu. Mwenzangu unagapi mfukoni? Nimeiweka hiyo picha mapema nirudi nyumbani kama afanyavyo kuku si unajua daladala za kibongo mpaka ulukie dirisha upate kochi la kulala.

Oyaa ona sasa!




Huo ndio utamu wa Mafunzo wakwanza aliyeshika tama ni Tuwene Mbelle, Reppotour wa semina TGNP na anayefuata ni Happy wa TGNP wakifuatilia Mada. Picha ya Pili kaka juma alishangaa Pilikapilika za waendesha Maguta toka mahakama ya ndizi pale mabibo hata hivyo alifurahia sana maandishi kuwa Kaza Buti.... sielewialiguswa na nini.
(Picha hizo zote mbili ni kwa hisani ya kaka Juma Nyumayo wa Ruvuma Press Club)

Mchoro huo ndio zawadi yangu ya kwanza kwako ujiandae kupata uhondo zaidi Hivi ndiyo Vionjo vya Bongo. (Mchoro na Muhidin Msamba)

Wabongo bwana kwa mishemishe!

Karibuni waungwana wa Bongo!

Hodi hodi wabongo! Nipo njiani kuwaletea Vionjo kama jina langu linavyoonyesha.
Pamoja na kuleta makandamizo hayo bado nitahitaji mchango wenu mkubwa katika ushauri, Kukosoa na mengine mengi.
Hata hivyo naomba kuwashukuru TGNP walioandaa semina ya Mafunzo kwa Wanahabari, Wasanii na wachora katuni katika Mafunzo ya Kijinsia kuleta Vuguvugu la Ukombozi wa wanawake waliopo pembezoni na kuniunganisha na Kaka Juma Nyumayo wa Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club toka Songea ambaye ameniwezesha kufungu Blog hii. Asante sana Brothers and Sisters. Well come and watch.